TMA WAONGEZA SIKU 5 KUMPELEKA KAZI ZAO
Mwenyekiti wa Tuzo za Muziki Tanzania, David Minja ametoa tamko rasmi la kuongeza muda kwa wanamuziki kuwasilisha kazi zao katika vipengele wanavyotarajia kuwania katika msimu huu.
Minja ameweka wazi kuwa wamefikia uamuzi huo kutokana na tatizo la kimtandao ambalo limeathiri mamilioni ya watu katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki, zoezi la uwasilishaji lilitarajiwa kufungwa Mei 12, 2024 saa 5:59 usiku hivyo litaendelea hadi Mei 20, 2024.
Comments
Post a Comment