KITENGE HAKIJAWAI KUMCHUCHA MTU
Katika ulimwengu wa mitindo ya mavazi ya Afrika, huwezi kukosa mavazi yaliyoshonwa kwa kutumia kitenge.
Kitenge kimekuwa ni vazi maalumu linalomtambulisha mwafrika yoyote anapokuwa amevaa mahali popote duniani.
Pia kitenge kinaweza kushonwa katika mitindo tofauti na kuvaliwa na watu wote, Watoto hata wakubwa wanawake na wanaume na kuonekana nadhifu machoni pa watu.
Kupendeza ni jambo kubwa, ambalo wanamitindo na watu wanaopenda Kwenda na wakati hulizingatia.
Kupendeza ni jambo kubwa ambalo wanamitindo na watu wanaopenda kwenda na wakati hupenda kuzingatia.
Vazi la kitenge pamoja na kumfanya mvaaji kupendeza na kuvutia lakini pia umletea mvaaji heshima pindi anapovaa vazi hilo na kuingia sehemu yoyote.
Vazi hilo linaweza kuvaliwa katika mikutano yoyote mikubwa, sehemu za ibada,kanisani kazini na hata katika sherehe mbalimbali hii ni kutokana na heshima ya kitenge.
Baadhi ya watu maaarufu wanaonekana wanavyotokelezea na vazi la kitenge huku wakijibebea heshima kubwa.
Miongoni mwa watu maaarufu lakini pia kuna viongozi wa serikali wabunge na mawaziri mbalimbali wamekuwa wakipendeza na valzi la kitenge.
Kwa kutumia kitenge unaweza kushona gauni shati la kiume na la kike, kaptura, suruali na suti, pia na kutengeneza viatu hata mikoba.
Mataifa ambayo yanasifika kwa kuwa na vizuri ni pamoja na Congo DRC,Nigeria na Ghana.


Comments
Post a Comment