RAIS DKT SAMIA KUONGOZA MKUTANO WA USALAMA


Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuongoza mkutano wa siku mbili wa Baraza la Usalama la Umoja wa Afrika huku Tanzania ikiwa Mwenyekiti wa Baraza hilo kwa mwezi mmoja wote wa May.


Akiongea leo Jijini Dar es salaama Waziri wa Mambo ya Nje January Makamba amesema kama Nchi imepewa fursa ya kuandaa kumbukizi ya miaka 20 l tangu Baraza hilo lianzishwe mwaka 2004 na sherehe hizo zitafanyika katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam

Amesema Viongozi mbalimbali wa Nchi za Afrika watahudhulia mkutano huo utakaoanza May 24 na 25 huku Rais wa Gambia, Msumbiji, Uganda na Marais wengine wastaafu wa Afrika wakiongozwa na Dkt. Jakaya Kikwete na Chisano wa Msumbiji wakialikwa katika mkutano huo wa Baraza la Amani la Umoja wa Afrika.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA