WAREMBO VYUONI WAANZA KUTIFUANA
Wanafunzi wa vyuo watakiwa kujitokeza katika kushiriki shindano la urembo ili kutimiza ndoto zao wakiwa wasomi.
Akizungumza na habari leo jijini Dar es Salaam, wakati wa ufunguzi wa shindano hilo, Mkurugenzi wa 'The Look ' Kampuni inayoandaa Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi amesema kupitia shindano la Urembo ngazi ya vyuo vikuu (MISS HIGHER LEARNING) imekuwa likiacha alama nzuri kwani mara 3 mfululizo limekuwa likitoa washiriki katika ngazi hiyo na kufanikisha Miss Tanzania hadi kufika Miss World .
Amesema anatambua kuwa urembo ni uongozi lakini haitoshi kukamilisha sifa za mrembo huyo ni lazima awe na ufahamu mzuri .
"Miss Tanzania 2023 ametokea ngazi ya vyuo vikuu hivyo ni kielelezo tosha kuwa Miss Higher Learning inatoa Warembo wasomi ambao wanaandaliwa kuja kusaidia jamii na Taifa kwa ujumla". amesema
Pia ameongeza kuwa jukwaa la Miss Tanzania limekuwa ni msaada mkubwa kwa sasa kuwatumia warembo katika nyanja mbalimbali ikiwemo kisiasa,sanaa pamoja na kijamii na Makampuni ili kusaidia kufanikisha lengo au kusudio la jambo lolote la Kimaendeleo .
Kwa upande wake Mwanzilishi wa Shindano hilo Adam Kundiya amesema shindano la mwaka huu litakuwa na Kipaumbele zaidi kutokana na alama iliyowekwa na Miss Tanzania 2023 Trace Nabukera na warembo wengine ambao walifika mchujo wa mwisho (Top 5).
Aidha ameeleza kuwa usahili utaanza rasmi Mei 25,2024 Katika Mgahawa wa Hug Mug Masaki Jijini Dar es Salaam ambapo amefafanua zaidi kuwa sifa za ushiriki ni kuwa na umri kuanzia miaka 18 hadi 23 ambapo kwa Wanafunzi waliomaliza 2022,2023,2024 nafasi imetokea kwa mwaka huu.
Kwa upande wake Mdhamini mpya wa shindano hilo kutoka Benki ya DTB Afisa uwezeshaji Dennis Rauya amesema kupitia benki hiyo imeingia rasmi kwenye mashindano hayo ili kumpa rasilimali fedha mrembo kuhakikisha anatumia fedha kutimiza project yake ambayo katika mashindano hayo ndio kielelezo tosha cha kumpeleka Mrembo kuingia katika kinyang’anyiro cha Miss Tanzania hadi kushiriki Miss world.

Comments
Post a Comment