BONGO MUVI STARTIMES YAWAPA NEEMA

 


Filamu zaidi ya 120  za wasanii wa Tanzania zimenunuliwa na chanel mpya ya St Swahili Plus chini ya Startimes Media kwa ajili ya kuoneshwa kwa watazamaji.

Akizungumza Dar es Salaam juzi kwenye uzinduzi wa chanel hiyo, Mkurugenzi wa Masoko na Maudhui wa Startimes David Malisa alisema hiyo yote ni kuunga mkono juhudi za wasanii katika kazi zao lakini pia,  kuhakikisha wanatoa burudani kwa Watanzania.

"Tumeanisha chanel ambayo silimia 60 ya Maudhui yanatoka ndani ya nchi. Tumetoa fursa kwa wasanii kwa kununua kazi zao ili na wao waweze kunufaika lakini pia na watazamaji wetu waburudike, jambo la muhimu tumekuja na kampeni ya kamatia furushi watu walipie vifurushi kuanzia sh 23000 wanufaike,"alisema.

Malisa alisema uzinduzi huo umeenda sambamba maudhui mengine ya chaneli nyingine mpya kama ST Toons, ST Toonie, ST Kids Plus, ST movies kwa ajili ya kuonesha vipindi mbalimbali vya tamthili, watoto nafilamu.

Mwakilishi wa Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita) Edward Nnko aliwapongeza Startimes kwa kutoa fursa kwa Watanzania akisema imekuwa ikitoa nafasi ya watu mbalimbali duniani kujifunza Kiswahili kupitia vipindi tofauti 

"Nawahimiza Watanzania waendelee  kukamatia fursa unaweza kusema sio Kamatia furushi tu, bali kamati fursa, elimu ya kujifunza, kuburudika na kwa uhakika watajisikia furaha,"alisema.

Mwakilishi wa wasanii Rashid Mrutu alisema  tangu 2018 wamekuwa wakikusanya   Maudhui mbalimbali ya filamu na wamehusika  kukusanya filamu nyingi za Kitanzania.


Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA