BASATA WAONGEZA MUDA WASANII KUJISAJILI





Katibu Mtendaji  wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Dk Keedmon Mapana ameongeza muda hadi Mei 30, 2024 kwa wasanii kuhuisha vibali vyao vya kufanya shughuli za sanaa nchini mara baada ya kupokea maombi kutoka kwa marais wa mashirikisho ya sanaa za ufundi, maonesho na muziki nchini

Ameyaongea hayo mbele ya waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Bwana Adrian Nyangamale ameahidi kutoa ushirikiano kwa kutemembelea wanachama wao waweze kutekeleza takwa la kiutaratibu lenye manufaa katika muendelezo wa shughuli za sanaa nchini.

Ikumbukwe wiki moja iliyopita Baraza lilitoa tamko lililowataka wasanii kuhuisha vibali vyao ndani ya siku saba kabla ya kuweka hadharani orodha ya wasanii wote ambao vibali vimepitwa na wakati.


Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA