FCS WAINGIA MKATABA NA LATRA CCC ULINZI WA USAFIRISHAJI


Foundation for Civil Society (FCS) na Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za za Usafiri Ardhini (LATRA CCC) wamesainiana Mkataba wa Makubaliano (MoU) wa miaka mitatu ili kuimarisha ulinzi wa walaji na haki zao ndani ya sekta ya usafiri ili kuwe na huduma bora kwa Wasafirishaji na wasafiri.


Akizingumza na Waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa FCS Justice Rutenge amesema kuungana kw FCS na LATRA CCC wanakusudia kuunda mazingira bora ya walaji katika sekta ya usafiri wa ardhi, kukuza taratibu bora za kibiashara na kuhamasisha ukuaji wa biashara.

Amesema ushirikiano huo unalenga kuwakilisha maslahi ya walaji wanaotumia usafiri wa ardhi ulio na udhibiti kwa ajili ya bidhaa na huduma katika nchini ambapo MoU itahakikisha wasafiri na wasafirishaji kwa njia ya ardhini wanapata huduma bora zenye kukidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa.



Pia  Ushirikiano huo wa kimkakati utahusisha kubuni na kutekeleza mipango inayokuza haki za walaji na kulinda bidhaa na huduma za usafiri wa ardhi zinazodhibitiwa.

Wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa Makubaliano, Mkurugenzi Mtendaji wa FCS alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kuimarisha uwezo wa raia na nguvu za ulinzi wa walaji.


Alibainisha kwamba ulinzi mzuri wa walaji katika sekta ya usafiri ni wa muhimu na alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wadau wa maendeleo, akisema kuwa ushirikiano huu utaimarisha mifumo ya ulinzi wa walaji na kuhakikisha kuna hatua madhubuti za kulinda walaji.







“Kadri Tanzania inavyosonga mbele kuelekea kukuza mazingira yanayosaidia juhudi za pamoja za kukuza taratibu za biashara zinazofaa na kuwapa walaji maarifa, FCS na LATRA CCC wanatarajia kutekeleza mpango mpana wa ulinzi na haki za walaji katika sekta ya usafiri nchini Tanzania, wakikuza uwezo wa walaji, kutetea haki zao na kuimarisha ushirikiano na wadau muhimu,” alisema.

Ulinzi wa walaji unabaki kuwa kipaumbele cha kimkakati kwa FCS, kama inavyoonyesha makubaliano yao ya hivi karibuni ya ufadhili wa miaka mitatu na Trademark. Ushirikiano na LATRA CCC unalenga kufikia malengo haya, kwa kuhusisha jamii na baraza la udhibiti kupitia ushirikiano na wadau muhimu na kuanzisha kamati za walaji maalum kwa ajili ya maeneo na sekta.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA