VILEMBA KINAVYO WATOA BOMBA WADADA



Na Brighiter David 

Karibu katika ya mitindo Leo tutaongelea viremba na kofia vinavyoweza kukufanya ukaonekana nadhifu huku ukienda na fashioni.

Awali ufungaji wa vilemba ulikuwa ukionekana zaidi misibani, makanisani na mashambani lakini sasa hali imebadilika tofauti na zamani.

Unaweza Kufunga kilemba ukaenda sehemu yoyote ile ya heshima hata kwenye mikutano mikubwa na  ukaonekana nadhifu.


Kungunga kilemba kwenye shughuli mbalimbali kulitokana na wenzetu wa nchini Nigeria na Congo walivyoamua kuendeleza utamaduni wao huo na kila kukicha kubuni mitindo mipya ya ufungaji wa vilemba.

Siyo wote tuna utaalamu wa kufunga vilemba licha ya kuwa tunapenda mtindo huo.

Kama tulivyoona Sio wote wenye uwezo wa kufunga vilemba hivi kwa ushadi wenye uwezo wa kufunga vilemba hivi kwa ustadi.

Wabunifu wa mitindo mbalimbali walipongeza utaalam kwa kutengeneza kofia za staili mbalimbali ambazo zinafanana na viremba.

Ukiangalia kwa haraka unaweza usitambue kama aliye mbele yako amefunga kilemba au amevaa kofia, hilo linatokana namna zilivyotengenezwa kisasa.

Kofia hizi zipo katika mitindo na rangi tofauti tofauti, na huvaliwa na kumpa fursa mtu kuchagua kulingana na matakwa yake.

Uzuri wa kofia hizi zinaweza kuvaliwa mahali popote na mvaaji akaendelea kuonekana wa kisasa tofauti na ilivyokuwa awali.

Ilikuwa nadra sana kumkuta mtu kavaa suti na kofia.

Hali imebadilika Mtindo huu wa kofia unakuruhusu kupangilia vazi lako la suti na kuendelea kuonekana nadhifu.

Unaweza pia kuvaa suruali yako ya kitambaa, jeans na blauzi utakayopenda kisha juu ukapiga kofia kulingana na rangi ulizochagua kutokana na rangi  za nguo ulizovaa.

Ukivaa nguo ya kitenge ndio mahala pake zinaendana sana na kofia au nguo ya rangi moja ukichanganya na kofia ya kitenge inanoga sana.

Ingawa kila mtu ana chaguo lake ila ukitaka kunoga zaidi ukivaa kofia hii uvae kiatu chenye kisigino kirefu kinakuongezea unadhifu katika mapigo yako.

Tukutane wiki ijayo katika makala ya urembo na mitindo usikose

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA