MIAKA 60 YA MSONDO NGOMA KUFANYIKA GWAMBINA
TAMASHA la Miaka 60 ya Msondo Ngoma Music Bandi Baba ya muziki wa Dansi linatarajia kufanyika Oktoba 26 mwaka huu katika viwanja vya Gwambina Lounge zamani TCC Club Changombe jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja wa bendi ya Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti, amesema kuwa bendi hiyo itaweka kambi ya wiki mbili mkoani Dodoma kwa nia ya kujifua zaidi.
"Msondo ngoma tuna jambo letu la Miaka 60 kuanzishwa tamasha la sasa litakuwa na vitu vizuri na ubunifu ndani ya miaka 10 iliyopita baada ya kuadhimisha miaka 60 wamejiunga wanamuziki wengi."
"Miaka 60 ya Msondo Ngoma Bendi itaanza na kisomo kitakachofanyika Oktoba 13 Hamana ofisini za bendi hiyo ikiwa ni sehemu ya kuwakumbuka waimbaji waliotangulia mbele za haki.
"Waimbaji wanafanya mazoezi ya kutosha siku hiyo wataimba 'live' ili kukonga nyoyo za mashabiki zao wanaoipenda Msondo Ngoma wakati wote wanapotoa burudani."amesema Kibiriti
Kwa upande wake Msanii Freshi Jumbe anayeishi nchini Japan aliyetamba na wimbo wa 'penzi ni kikoozi amesema kuwa ni miongoni mwa waimbaji wa bendi ya Msondo na ameimba nyimbo nyingi atazifanyia mazoezi na ataimba siku hiyo.
Ally Choki amesema kuwa siku hiyo ataimba wimbo alioimba na Mzee Ngurumo Baba ulichomtendea Mama pamoja na husia wa wazazi.
Naye Juma Katundu maarufu kama 'JK' amesema kuwa ni kitu kikubwa kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na kutoa ushirikiano siku hiyo
Tamasha la Miaka 60 ya Msondo litasindikizwa na Twanga Pepeta, Ally Choki, Nyoshi El Sadati Rais wa Milele, Spidoch Band 'Wazungu weusi' pamoja na msanii wa Bongo fleva Bernard Paul 'Ben Paul'.
Tamasha la miaka 60 kiingilio ni Laki moja, Elfu 50 na kawaida 15000 ukichukua tiketi yako mapema kwa mlangoni kiingilio ni Elfu 20.



Comments
Post a Comment