USAILI WA BSS KUANZA ARUSHA NO 9 NA 10

 

USAHILI wa Wasanii wa Shindano la  Bongo Star Search African kuanza kufanyika Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 katika ukumbi wa SG Resourt Mianzini.


Akitaja maeneo ambayo usahili utafanyika wa Bongo Star Search African Madam Ritha amesema kuwa Usaili utaanza Arusha na baadaye Mkoani Mwanza.

"Mkoani Arusha Novemba 9 hadi 10 2024 SG Resourt Mianzini, Mwanza Novemba 16 hadi 17 mwaka huu La Kairo  Hotel, Kampala Novemba 23 hadi 24 mwaka huu, Nairobi Novemba 30 hadi 01DEC 2024 Little Thiether Babati Desemba 6 hadi 7 Olympic Lounge huku Dar es Salaam ikiwa Decemba 13 hadi 15, 2024 katika ukumbi wa Makumbusho ya ya Taifa Bongo Star Search Afrika!

Madam Ritha aliongeza kwa kuwashukuru wadhamini kwa kuendelea kuwa shika mkono kwa juhudi wanazofanya kuendelea tasnia ya burudani nchini.

"Kwa wadhamini wetu na washirika wa Bongo Star Search, tunatoa shukrani.
Hamjawa tu wadau, bali ni sehemu muhimu ya mafanikio ya mpango huu. Ushirikiano wenu umetufanya kufikia malengo haya ya kupanua wigo na kufikia zaidi ya mipaka ya Tanzania.

Mashindano hayo yataonyeshwa kupitia vyombo mbali mbali vitakazo kuwa vinaonesha kipindi chetu moja kwa moja 
Tanzania: St Swahili Channel ndani ya Star Times Uganda: Makula Tv 
Nairobi: St Swahili ch 160 & 400

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA