VIJANA WA TANZANIA HAWAPO TAYARI KUISHI BILA AMANI

Steve Nyerere: Vijana msishiriki maandamano, tulinde amani ya taifa – Dar es Salaam Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanae, Steve Nyerere, amewataka vijana nchini kujiepusha na maandamano na badala yake kushikamana kulinda amani na utulivu wa taifa. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve alisema Tanzania imekuwa mfano wa nchi zenye amani barani Afrika, hivyo vijana wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuilinda na kuienzi hali hiyo. “Mtanzania yeyote hana tabia ya kuandamana, bali kushikamana. Nchi yetu ina amani ambayo imejengwa kwa muda mrefu; ikipotea, kuirudisha ni jambo gumu sana,” amesema Steve. Aliongeza kuwa vijana wanapaswa kuelekeza nguvu zao katika kujenga uchumi, kushiriki shughuli za maendeleo na kuunga mkono juhudi za serikali zinazoendelea kuimarisha amani, umoja na mshikamano wa kitaifa. “Vijana ndio nguvu ya taifa, tuitumie vizuri nguvu hiyo kwa manufaa ya taifa letu, siyo kujiingiza katika mambo yanayoweza kuvuruga amani,” ameisitiza.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA