GOZBERT AFUNGUKA SABABU ZA KUCHOMA GARI MOTO

Goodluck Gozbert afunguka sababu ya Kuchoma gari la zawadi sio nyota Msanii wa muziki wa Injili, Goodluck Gozbert, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu tukio la kuchoma gari alilokuwa amepewa kama zawadi na Nabii Mkuu Geordavie, akisema kuwa uamuzi huo ulikuwa wa makusudi kwa ajili ya ukuaji wake wa kiroho na kimaisha. Akizungumza kwa hisia, Gozbert amekanusha vikali uvumi ulioenea mitandaoni kuwa gari hilo lilichomwa kutokana na madai ya kuchukuliwa nyota yake. Ameeleza kuwa hatua hiyo ilitokana na safari yake binafsi ya kujitambua na kutaka kuendelea mbele zaidi katika maisha. "Kila binadamu anakuwa, kila binadamu anagrow. Asa asiyejiangalia muelekeo wake au asiyejua anaelekea wapi baada ya muda fulani, ni aina ya watu utawakuta miaka yote wako vile vile, wapo pale pale. Bahati mbaya sana mimi siyo wa namna hiyo," amesema Gozbert. Ameongeza kuwa alikuwa na hamu ya kuona mabadiliko makubwa katika maisha yake na kuchukua hatua kubwa ya kujitenga na vitu vilivyokuwa vinamrudisha nyuma mojawapo ikiwa ni gari hilo. "Kwa hiyo, kwa sababu kukua ni kitu ambacho ni moja ya vitu nilivyokuwa navitamani, ndiyo kitu ambacho kilitokea kwenye maisha yangu," ameongeza. Hatua hiyo imeibua maoni tofauti mitandaoni, baadhi wakimpongeza kwa ujasiri na msimamo wake, huku wengine wakibaki na maswali kuhusu undani wa uamuzi huo. Hata hivyo, Gozbert anasisitiza kuwa yeye ni mtu anayejua anachokitaka na hayuko tayari kubaki sehemu moja maishani.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA