UDSM YATEKELEZA MRADI WA HEET ELIMU KIDIGITALI
Na Brighitte, Dar es Salaam
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinaendelea kutekeleza kwa mafanikio Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Uchumi (HEET), ambao unalenga kuboresha miundombinu, kuimarisha mitaala, na kuendeleza mfumo wa kujifunza kwa njia ya kidijitali.
Mradi huo wa kimkakati una umuhimu wa kitaifa katika kubadilisha elimu ya juu kuwa chachu ya uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya Taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye, alisema mradi wa HEET ni mpango wa kitaifa unaotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa thamani ya Dola za Marekani milioni 425.
“Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha mazingira ya kusomea na kuhakikisha mitaala ya vyuo inalingana na mahitaji ya soko la ajira,” amesema Prof. Anangisye.
Aliongeza kuwa chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, UDSM imetengewa kiasi cha Dola milioni 49.5 (sawa na Shilingi Bilioni 121) kwa ajili ya kutekeleza mradi huo kwa kipindi cha miaka mitano (Julai 2021 – Juni 2026).
Malengo mahususi ya MRADI WA Heet kwa UDSM niUtekelezaji wa mradi huo katika UDSM umejikita katika maeneo makuu sita:Kuboresha Miundombinu ya Kufundishia na Kujifunzia – Ujenzi wa madarasa, maabara, karakana na vituo vya kujifunzia kwa njia ya kidijitali, ikiwemo ujenzi wa kampasi mpya mkoani Lindi (Ngongo na Ruangwa) na Kagera.
Maboresho ya Mitaala – Kuoanisha mitaala na mahitaji ya soko la ajira, viwanda na jamii.Kujengea Watumishi Uwezo – Ufadhili wa masomo ya uzamivu na umahiri kwa wahadhiri.
Mabadiliko ya Kidijitali – Kuimarisha miundombinu ya TEHAMA na mifumo ya ujifunzaji kwa njia ya mtandao.Utafiti na Ubunifu – Kukuza ushirikiano kati ya chuo na sekta binafsi katika ubunifu na biashara ya teknolojia.Utawala Bora na Ujumuishi – Kuboresha mifumo ya uwajibikaji, usawa wa kijinsia na uendelevu wa taasisi.
Mafanikio yaliyopatikana hadi sasa Prof. Anangisye alisema UDSM imefikia asilimia 80 ya utekelezaji wa mradi huo, huku mafanikio makubwa yakiwa yamepatikana katika maeneo mbalimbali.
Kupitia HEET, chuo kimeanzisha miradi mikubwa ya ujenzi, ikiwemoKampasi mpya Lindi (majengo tisa) na Kagera (majengo matatu)Majengo 11 mapya ya kufundishia na ofisi za wahadhiri yaliyofikia asilimia 75 ya ujenziHosteli za wanafunzi wa shahada za uzamili na shahada za kwanzaKituo cha huduma za jinsia na mahitaji maalumuUkarabati wa majengo ya CoET (Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia).
Mabadiliko ya KidijitaliUDSM imeboresha miundombinu ya mtandao kutoka uwezo wa 1.5Mbps hadi 10Mbps, na kufunga vifaa vya kisasa vya kufundishia kwa wanafunzi zaidi ya 8,000 kwa wakati mmoja.
Zaidi ya masomo 1,000 yameingizwa kwenye mfumo wa e-learning, huku wanafunzi 39,000 (wakiwemo 165 wenye mahitaji maalum) na wahadhiri 600 wakitumia mfumo huo.
Maboresho ya Mitaala Chuo kimefanyia mapitio mitaala 250 ili iendane na soko la ajira, ikizingatia kuongeza muda wa mafunzo kwa vitendo na kuimarisha umahiri wa wahitimu.
Uendelezaji wa Rasilimali Watu Wanataaluma 29 wamefadhiliwa kusoma katika ngazi za Uzamivu na Umahiri katika vyuo vikuu vya kimataifa, kati yao asilimia 30 ni wanawake.
Ushirikiano na Sekta Binafsi UDSM imeanzisha Kamati za Ushauri za Kitasnia na kusaini makubaliano na makampuni 24 kwa ajili ya mafunzo kwa vitendo (internships) na ubadilishanaji wa uzoefu wa kazi kwa wahadhiri.
UDSM imejipanga kuendeleza mafanikio ya HEET hata baada ya kipindi cha ufadhili kumalizika kwa, Kujumuisha shughuli za mradi katika bajeti ya kawaida ya chuo, Kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi na wadau wa kimataifa, Kukuza mapato kupitia ubunifu na tafiti, Kuendeleza mfumo wa elimu ya mchanganyiko (blended learning).
Kwa ujumla, mradi wa HEET umeifanya UDSM kuwa kinara wa mageuzi ya elimu ya juu nchini Tanzania, sambamba na utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 na mpango wa Tanzania ya Kidijitali chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kwa upande wake Naibu Mratibu wa Mradi wa Heet (UDSM) Prof Libelato Haule amesema faida za Mradi wa HEET Kuimarika kwa ubora wa elimu kutokana na mitaala na vifaa vya kisasa Kuongezeka kwa upatikanaji wa elimu kupitia mfumo wa e-learning Kuongezeka kwa ajira kwa wahitimu zaidi ya asilimia 82 hupata ajira ndani ya mwaka mmoja Kuimarika kwa hadhi ya UDSM kimataifa.
Mradi huu umenufaisha makundi mbalimbali, yakiwemo wanafunzi, wahadhiri, sekta binafsi na jamii kwa ujumla kupitia utafiti, teknolojia mpya, na ajira zinazotokana na ubunifu wa ndani



Comments
Post a Comment