UWAZI WA FEDHA KATIKA NDOA WADUMISHA UPENDO

Mchungaji Dkt. Christine Mbelwa: Wazi wa Fedha Katika Ndoa Wajenga Maelewano
Mchungaji Dkt. Christine Mbelwa amewashauri wanandoa kuwa wawazi kuhusu masuala ya kifedha ili kusaidia kuimarisha uhusiano na kusaidiana katika kuhudumia familia.
Akizungumza na Habari leo kwenye semina ya wanandoa iliyoandaliwa na PIMEA Dkt. Christine amesema kwamba uwazi wa kifedha baina ya wanandoa unasaidia kujenga uaminifu, kuelewana na kushirikiana kwa karibu katika kupanga na kutekeleza majukumu ya kifamilia.
“Ni muhimu kila mmoja kujua kipato cha mwenzake. Sio mwanamke anaficha kipato chake huku mwanaume pekee ndiye anayebeba mzigo wa familia,” amesema.
Ameongeza kuwa fedha zisipangiwe kwa siri, bali zitumike kwa ushirikiano, huku kazi, ratiba, na changamoto za kila siku zikifahamika kwa wote wawili. Pia, amesisitiza kuwa matatizo yashirikishwe mapema kabla hayajazidi kuwa makubwa.
“Mshikamano wa kifedha hujenga msingi imara wa ndoa yenye afya na maelewano ya kweli,” amehitimisha.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA