HUYU HAPA WEMA SEPETU WA MAMA SAMIA
Mwigizaji nyota nchini WemaSepetu ametangaza hatua za kampeni yake ya kitaifa 'Wema wa Mama' inayolenga kuonyesha mafanikio makubwa ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kupitia usahidi wa picha kila hatua kwa makala mbalimbali watazamaji watapata fursa ya kusikia moja kwa moja kutoka kwa wananchi waliofaidika na miradi ya serikali.
Aidha, Wema Sepetu pia kwa atazungumza na kujionea miradi mikubwa ya maendeleo katika sekta za maji, afya, na elimu kwa lengo lingine la kuelewa namna fursa za maendeleo zilivyoanzishwa na zinavyohitaji nguvu kazi, uwekezaji, na ushirikiano wa wananchi.
Kampeni hii inaadhimisha juhudi na mafanikio ya serikali, ikiwemo maeneo ya kipaumbele kama vile miundombinu, afya, elimu, na kilimo. Lengo ni kuhamasisha, kuunganisha na kuongeza ari ya maendeleo katika jamii nzima ya Watanzania.


Ok
ReplyDelete