WATAALAMU WA AFYA KUSHIRIKI MKUTANO WA MAGOMJWA YA MOYO ZANZIBAR
WATAALAMU wa afya 500 kutoka nchi mbalimbali Duniani wanatarajia kukutana ili kufanya Mkutano wa kimataifa wa tatu wa magonjwa ya Moyo utakaoangazia namna bora ya kuimarisha matibabu ya moyo.
Mkutano huo utafanyika Visiwani Zanzibar
Aprili 10 hadi 12,2025 ambapo watoa mada 60 watawasilisha mada zao huku Mgeni rasmi akiwa ni Rais Samia Suluhu Hassan ambaye atawakilishwa na Makamu wa pili wa rais wa Zanzibar Hemed Suleiman.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)Dk Peter Kisenge amesema mkutano huo utaangalia maendeleo ya karibu katika kuimarisha matibabu ya magonjwa ya moyo ikiwa ni tiba,upasuaji na kujikinga.
"Utakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya afya na viongozi ndani na nje ya nchi na vilevile rais wa chama cha Moyo cha Marekani atakuja na Chama cha moyo cha Ulaya, malengo ni kujadiliana matibabu ya moyo mapya lakini tunataka kuchochea tiba utalii ambayo itakuwa na matokeo chanya,"amesisitiza Dk Kisenge.
Aidha ameeleza kuwa miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika mikutano iliyopita ni kupataa ujuzi na baadhi ya wagonjwa walifanyiwa upasuaji JKCI ambao ni wa kisasa zaidi.
"Tulitengenezaa mahusiano ya masuala ya utafiti tumendika maandiko matatu ya kufanya utafiti na tunategemea kupeleka baraza la utafiti Marekani ili kupata fedha,andiko moja wapo ni jinsi ya kuzuia magonjwa ya moyo kwa watu wanaotumia sigara hili limeshaenda.
Ameongeza " Na pili ni andiko la tiba mkoba ya Dk Samia Suluhu Hassan ili tupate hela ya kufata wananchi na tatu ni shikizo la damu tutafanya tafiti kuhusu hili na pia madaktari wetu wameenda kusoma Afrika Kusini.
Amesema kumekuwa na ongezeko la utalii wa matibabu kutoka watu 150 hadi watu 600 baada ya kujua kinachofanyika hasa upasuaji.
"Tunapata kutoka nchi za Congo,Malawi,Comoro,Zambia,Seir lion na wa Poland,Norway na zingine wakija kufanya utalii wakapata tatizo wanaletwa hapa.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tiba ya Moyo,Dk Tatizo Waane amesema mkutano huo unalenga kuimarisha matibabu ya moyo kwa pamoja barani Afrika.
"Kupitia mkutano huu JKCI imejulikana Duniani na hivi karibuni tulipata tuzo ambapo daktari wetu alipewa na amepata nafasi ya kupata mafunzo matibabu ya moyo na haya ni matunda ya uwekezaji wa serikali.
Amesema faida nyingine kutokana na mafanikio nchi zingine zinakuja kujifunza jinsi ya kutoa huduma za moyo kama Zambia,Kenya na Burkina Faso.
Naye Kaimu Mwenyekiti wa Mkutano huo,ddi Lemali ametoa rai kwa wale ambao hawajajiandikisha wajiandikishe katika website ya www.teamafrica.or.tz au namba 0761699776.
Kwa upande wake Daktari aliyepewa tuzo
Dk Khuzeima Khanbhan amesema pia anatarajia kuhudhuri mafunzo ya mwezi mmoja nchini Marekani ikiwa ni sehemu ya ushindi wa tuzo hiyo.
"Mkutano wa moyo ni muhimu Kwani tutakutana na watu mbalimbali duniani kufanya,kujadili,kubadilisha ujuzi kuhusu matibabu ya moyo.
Mwishooo....



Comments
Post a Comment