ONYO KALI USIPOSTI PICHA YA MTOTO AU MTU YOYOTE BILA RUHUSA
Usiposti Picha za Wengine Bila Ridhaa – Polisi Watoa Onyo Kali
Dodoma – Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Wilfred Willa kutoka Kitengo cha Dawati la Jinsia, Ulinzi na Mtoto, Makao Makuu ya Polisi Dodoma, amewaonya wananchi dhidi ya tabia ya kuposti picha za watu wengine mitandaoni bila ridhaa yao, akibainisha kuwa kitendo hicho ni kosa la kisheria.
Akizungumza katika mahojiano maalum, Willa amesema kuwa mtu yeyote anayeposti au kusambaza picha ya mtu mwingine mitandaoni bila idhini, anavunja Sheria ya Makosa ya Mtandao, kifungu cha 23 cha s
heria namba 14 ya mwaka 2022. Sheria hiyo inalenga kulinda haki ya faragha ya mtu na kuzuia matumizi mabaya ya picha au taarifa binafsi kwenye mitandao ya kijamii.
“Kosa hili linaweza kumgharimu mtu kifungo cha hadi miaka mitatu jela, faini ya Shilingi milioni tano, au adhabu zote kwa pamoja,” amesema Willa.
Ameeleza kuwa watu wengi hawajitambui kuwa wanakiuka sheria wanapochukua na kusambaza picha za watu wengine mtandaoni bila ruhusa, jambo linaloweza kuwasababishia matatizo ya kisheria.
Kwa upande wa watoto, Willa amesisitiza kuwa kuna ulinzi wa kisheria wa kiwango cha juu zaidi, na kwamba wazazi au walezi wanapaswa kuwa makini kabla ya kuposti picha za watoto wao mitandaoni, wakizingatia usalama, heshima na faragha ya mtoto.
Amewataka wananchi kuwa na tahadhari kubwa katika matumizi ya mitandao ya kijamii, hasa kuhusu matumizi ya picha za watu wengine, na kuhakikisha kuwa ridhaa imepatikana kabla ya kusambaza au kuposti chochote mtandaoni.


Comments
Post a Comment