SBC TANZANIA YAINGIA MAKUBALIANO NA PIZZA HUT

Mazingira mazuri ya uwekezaji yaliyowekwa na serikali nchini yamechochea Kampuni ya SBC Tanzania kuingia makubaliano ya kibiashara na Pizza Hut. Makubaliano hayo yamewekwa katika hafla fupi iliyofanyika Pizza hut Mbezi jijini Dar es Salaam Leo.
Meneja Masoko wa SBC Tanzania Jasper Maston ameishukuru serikali kwa kuwapa fursa ya kufanya biashara kwa amani na kuweka mazingira rafiki ya kuwafikia wateja wao kiurahisi. “Tunashukuru serikali kwa kutupa fursa nzuri na njia sahihi kuhakikisha tunafikisha huduma zetu kwa urahisi zaidi, kuwafikia wateja wetu na kuweza kuwa namba moja Tanzania,”amesema.
Amesema muungano huo kupitia kinywaji chao cha Pepsi umelenga kuwafikia wateja wao kwa urahisi. Kwa upande wake, Meneja Rasilimali Watu wa Pizza Hut Sixberty Malya amesema walianza biashara ya Pizza wakiwa na mgahawa mmoja lakini sasa wana migawa mingi Dar es Salaam na Arusha na wameajiri mamia ya vijana wa Kitanzania. Amesema mpango wao mwingine ni kufika mikoa yote lakini kwanza jiji la Dodoma na kuendelea kutengeneza fursa nyingine za ajira. “Na hii ni kutokana na mazingira yaliyotengenezwa na serikali iliyopo chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, ametuwekea mazingira mazuri ya kibiashara na sisi tunazidi kupanuka kibiashara,”alisema. Alisema mipango kwa ushirikiano na SBC anaamini hivi karibuni watafungua matawiki katika mikoa mbalimbali nchini na miongoni mwao ni Dodoma, ambako kumekuwa na usafiri wa haraka. “Dodoma usafirishaji ni rahisi kutokana na vitu tunavyotumia katika uandaaji wa Pizza, muda sio mrefu tunatarajia kuwafikia na wao wanufaike na huduma zetu,”alisema. Mwisho

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA