MOSE IYOBO HAKUNA WA KUNITENGA NA COOKIE
Dansa kwenye video za wasanii wa Bongo fleva Moses Iyogo 'MoseIyobo' amesema kuwa hakuna mtu anaweza kuchukua nafasi yake kwa mwanae Cookie hapa duniani.
Akijibu swali kuhusiana na mwanae kupewa zawadi ya gari huku yeye akitumia muda nae mwingi kufundisha kucheza nyimbo za wasanii, amesema kuwa atabaki kuwa baba Cookie tu.
"Baba ni baba hakuna anayeweza kumbadili mtu kuwa mzazi wa Fulani na kuhusu gari aliyozawadiwa na mama yake Cookie sidhani kama anapanda hiyo gari chunguzeni vizuri mtapata majibu."
"Hakuna zawadi nzuri duniani kwa mzazi kumpa mwanae kama Upendo ni kitu kikubwa sana kwa kumpa mtoto wako, Kuna watoto wamekosa upendo wa wazazi ndio sababu nampatia mwanangu."amesema Mose
Aidha ameongeza kuwa "hakuna kitu kinachoweza kutenganisha mtoto na mzazi wake kwa namba yoyote Cookie niwanangu nampenda na ananipenda."
"Ninachojua natimiza majukumu yangu kama mzazi kuhusu huo zawadi gani nimpatie mwanangu sipangiwi na mtu nimpe nini mwanangu."amesema Mose


Comments
Post a Comment