HAMISA NIPO SINGO AZIZI KI SIO MPENZI WANGU
MREMBO na mwanamitindo, Hamisa Mobetto amesema kwa sasa hana uhusiano wa kimapenzi na mwanaume yoyote.
Hamisa amesema kuwa ameamua kujipa muda na kufanya kazi zake hadi hapo atakapoamua tena kuingia kwenye mapenzi.
Pia amekanusha madai ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mcheza soka wa timu ya Yanga Aziz Ki.
“Sidhani kama kuna mishikano kama baadhi ya watu mnavyosema tulivyoonekana, chochote kilichokuwa kinaendelea pale ni cha kawaida, kama ungeniona na mtu mwingine mimi nipo singo nimeamua kujiba muda“
Ikumbukwe kuwa taarifa za Mobetto na Aziz KI kuhusishwa kimapenzi yalianza baada ya Hamisa kujumuika na wachezaji wa Yanga walipokabidhiwa Kombe la Ligi Kuu ya NBC uwanja wa Mkapa.


Comments
Post a Comment