TAMASHA LA HIP HOP ASILI KUFANYIKA PWANI


Msanii wa muziki wa HipHop Asili Festival kwa kushirikiana na ubalozi wa Ufaransa umeaanda tamasha la kimataifa la  Hip Hop asili lenye lengo la  kukuza utamaduni na ushirikiano likionyesha uridhi wa kipekee wa sanaa 

Tamasha hilo litafanyika Mkoani Pwani Bagamoyo katika Chuo cha sanaa cha TASUBA ambapo kutakuwa na muunganiko wa talanta za kitaifa na kimataifa katika utamaduni wa HiP HoP

Hayo ameyasema Ofisa Matei Babis Mkurugenzi wa Hip Hop Asili jana usiku kwenye Mkutano na waandishi wa habari ulifanyika Jijini Dar es salaam

Matei Amebainisha kwa kusema kutakuwa na asili band ambapo wanamuziki na wasanii wa kughani mashairi wameshirikiana kuunda mchanganyiko wa pekee wa hiphop lakini pia kutakuwa na upigaji midundo  kwa mdomo yaani ( Beatbox)

Ameongezea kuwa mbali na hayo kutakuwa na kutambulishwa kwa  (Breaking )kama mchezo wa Olimpiki pamoja na maonyesho ya sanaa ya machata (Graffiti) ambapk kuta za TASUBA zitapendezeshwa kwa usanifu wa graffiti kutoka kwa Wachata Tanzania na Kactus kutoka Ufaransa.

Nae Ofisa utamaduni na michezo ubalozi wa ufaransa Ettenne Pellausy amesema wameunga mkono tamasha hilo ili kukuza na kusapoti utamaduni wa sanaa husasani kwa wanawake

Nae Msanii wa Hip Hop nchini Tanzania Ibrahim Ayoub maarufu Country Wizzy atakakuwa kwenye tamasha hilo amesema mziki huo wa Hip Hop umeonekana hauna nguvu lakini kupitia tamasha hilo litakuza mziki huo na kuwapa thamani wasanii kwenye Stage kubwa 

Tamasha hilo ni la nne kufanyika na lilianza mwaka 2021 ambapo miongoni mwa wasanii watakaokuwa kwenye tamasha hilo ni Maalim Nash, Country Wizzy,Machalii watundu,Sinaubi Zawose na Casey kutoka Ufaransa.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA