MTANDAO WA X KUFUNGIWA TZ


Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) umeiomba Serikali kupitia Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kuufungia mtandao wa Twitter (X) kutokana na maudhui yake kutokuendana na mila na desturi za kitanzania .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Amesema dhamira ya maudhui ya mtandao wa Twitter maarufu X kwa sasa ni mbaya kutokana na kutokwendana na tamaduni za kitanzania.

“UVCCM imekuwa na utamaduni na kazi ya kuendelea kufatilia malezi ya vijana wa kitanzania wote ambapo hivi karibuni imepokea taarifa kuwepo Kwa mtandao wa X wenye maudhui ya kingono,” amesema.

Kawaida amesema kupitia Serikali Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa ikifungia mitandao yote yenye maudhui ya namna hiyo hivyo anaimani pia itaufungia mtandao huo.

“Sasa wakati umefika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuufungia mtandao huo kutokana na maudhui yake kutokwendana na mila na desturi zetu “

"Huu ni mwanzo tumeanza na mtandao wa X Twitter mingine  kama itakuwa ya aina hii nayo pia itafata hatutaki kuharibi maadili yetu."amesema Kawaida

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA