MAMIA WAJITOKEZA KUPATA HUDUMA ZA MSAADA WA KISHERIA


Mamia ya Wananchi wa Wilaya ya Kinondoni na maeneo ya Jirani wamejitokeza kwa wingi kupata huduma ya msaada wa kisheria bure iliyotolewa na Shirika la Citizen Foundation kwa kushirikiana na Mama Samia legal Aid Campaign katika viwanja vya Tanganyika Packers - Kawe Jijini Dar-es-Salaam.

Akizungumza wakati wa utoaji wa huduma hiyo leo tarehe 22 - Juni 2024;  Mkurugenzi wa Mama Samia legal Aid Campaign Bi. Ester Msambazi amesema Wananchi wamejitokeza kwa wingi hali inayoonesha kuwa ipo haja kwa watoa huduma za msaada wa kisheria kuwafuata Wananchi badala ya kuwasubiria maofisini.

Amesema “Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ni namba moja katika utoaji wa huduma za msaada wa kisheria kwani yeye ndiye kiongozi wetu pale juu kwenye huduma hizo lakini Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Pindi Chana, katibu Mkuu Bi. Mary Makondo lakini na wadau wengine ambao ni Wanawake wanaonesha juhudi za pamoja kama Wanawake katika kuunga mkono  juhudi za Mhe Rais  Dkt. Samia kuhakikisha kila Mwananchi anaweza kufikiwa na haki anaipata kwa wakati na kwa ufanisi’’.

Kwa upande wake  Mkurugenzi wa Shirika la Citizen Foundation Bi. Lilian Wassira  amesema leo wamezindua Kliniki ya msaada wa huduma ya kisheria kwa Wananchi wakazi wa Wilaya ya Kinondoni ikiwa ni mwendelezo baada ya kuwa zoezi hilo limeshafanyika katika Wilaya za Temeke na Kigamboni kwa mafanikio makubwa.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wananchi waliojitoleza kupata huduma hiyo wameshukuru na kupongeza hatua ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kusogeza huduma ya msaada wa kisheria  waliopo Wananchi kwani imekuwa msaada mkubwa hasa kwa wasiokuwa na uwezo kumudu gharama za Wanasheria.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA