MADADA POA WAFIKISHWA MAHAKAMANI
WATUHUMIWA 24 kati ya 36 waliokamatwa Kwa kosa la kuuza miili yao maarufu kamà "dada poa" wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Sokoine Drive wakikabiliwa na tuhuma za kufanya vitendo venye mazingira ya umalaya.
Akizungumzia mazingira ya shauri hilo baada ya kutajwa, Wakili anayetetea kundi Hilo ,Peter Madeleka amesema Kwa sababu ambazo hazijafahamika watuhumiwa hao pekee ndio walifikishwa Mahakamani hapo.
Amesema watuhumiwa 18 wamefikishwa mbele ya Hakimu Janeth Mgaya na baada ya kusikiliza maelezo upande wa serikali,Hakimu alisema shauri liko wazi Kwa dhamana Kwa ajili ya washtakiwa wote 18 kwa dhamana ya Kila Mmoja kutoa fedha taslimu sh 300,000.
Madeleka amesema pamoja na dhamana hiyo lakini inadaiwa kuwa Hakimu alikuwa na dhamira ya kuona Haki inakwama na kwa mujibu wa Ibara ya 13(c) na (b) ya Katiba yeye mwenyewe ameamua kuwalipia dhamana watuhumiwa 18 kwa kiwango Cha sh milioni 5.4.
Aidha amesema watuhumiwa wengine watano,wamepewa sharti kuwa Kila mtuhumiwa anastahili kudhaminiwa na wadhamini wawili wenye barua za serikali za mitaa na kitbulisho Cha Taifa ambao walitimiza masharti na kuwa huru.
Amesema shauri hilo litasikilizwa kesho (Juni 26) katika Mahakama hiyo na kuwataka wapenda haki kufika Mahakamani Ili kupata fursa ya kujua suala la kuuza mwili linafanyikaje na nami mnunuaji na iwapo kama serikali inapata kodi.
Msako wa kuwakamata watuhumiwa hao ilifanyika hivi karibuni katika wilaya ya Ubungo,ikiendeshwa na Mkuu wa Wilaya hiyo ,Hassan Bomboko akiwa na askari polisi.

Comments
Post a Comment