SILENT OCEAN CONSUMER CHOICE AWARD AFRICAIMEZINDULIWA RASMI
Tuzo za Chaguo la Wateja Afrika (CCAA) litashirikisha biashara na chapa kutoka nje ya nchi, linatarajiwa kufanyika mwaka huu Novemba katika ukumbi wa The Super Dome.
CCAA pia inajulikana kama Silent Ocean Consumer Choice Award Africa ni chachu ya kupaza sauti za watumiaji na kuridhika na huduma na bidhaa mbalimbali sokoni.
Ni jukwaa la Afrika la utambuzi wa biashara na ushirika kwa watoa huduma wa bidhaa na huduma kupitia kura za watumiaji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuzindua msimu mpya Mwanzilishi na Mkurugenzi wa CCAA, Diana Laizer, alisema kuwa wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini, Kenya, Malawi, Nigeria, na nchi nyingine wanatarajiwa kuteua chapa zao katika hafla ya inayotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu."Tukio la mwaka jana lilikuwa na vipengele vikuu 22 na vijamii 70 katika mkutano huo. Vipengele hivyo vinajumuisha vifaa, mawasiliano ya simu, usafiri wa anga, huduma za kifedha, mali isiyohamishika, bima, mafuta na gesi, hoteli na ukarimu, usalama, bidhaa za walaji zinazokwenda kwa kasi, matukio na mapambo, mitindo na muundo, na upigaji picha.
"Ni wakati muafaka wa makampuni na chapa kushiriki na kuwashirikisha wateja wao wakati wa kampeni ya tuzo za mwaka huu," alisema Laizer.
Alisema anatarajia tuzo hizo zitaongeza ushindani na kuwapa motisha wajasiriamali, hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
“Tangu kuanzishwa kwa tuzo hizi tumeona mafanikio makubwa ambapo jumla ya washiriki 650 wa tuzo hizo za mwaka jana, niwanufaika” alisema Laizer.
Alitaja wanatarajia kuwa na mfumo mzuri na kwamba washindi watachaguliwa kwa kuzingatia vigezo na ubora wa bidhaa zao.





Comments
Post a Comment