VEE KASHERA HAKUNA WA KUNITENGANISHA NA AZIZI KI
MSANII wa Filamu za kibongo, Vanessa Kashera maarufu 'Vee Kashera' ameibuka na kudai kwamba mwanamitindo Hamisa Mobetto hawezi kuvunja mahusiano yake na kiungo mshambuliaji wa Yanga, Stephane Aziz Ki sababu kila mtu ana nafasi yake kwa mchezaji huyo.
Vee Kashera amesema Aziz Ki, mtu wake wa karibu na mahusiano yao ni urafiki sio kama watu wanavyosema juu ua kiungo huyo kwa wako kwenye mapenzi.
"Mashabiki ndio wanaozusha kuwa ni wapenzi hakuna sehemu tuliyoweka wazi jambo hilo kokote, hakuna mtu anaweza kuchukua nafasi yangu kwa Aziz Ki kila mtu ana urafiki wake kwa nafasi yake, nina muda wangu kwa Aziz K na Hamisa atakuwa na muda wake." Amesema mrembo huyo
Kuhusu kwenda uwanja wa Benjamini Mkapa siku Yanga wakikabidhiwa kombe, amesema hakujisikia kwenda kwenye sherehe za kukabidhiwa za ubingwa sababu alikuwa na mambo yake mengine.
"Nilikuwepo kwenye siku ya kuzaliwa kwa Hamisa alikuwepo kwenye sherehe za Yanga, sikutaka kwenda yule dada alienda Azizi KI ana marafiki wengi ndio ikiwemo huyo msaani mwenzangu ndio sababu ya kwenda kushuhudia sherehe hizo, " amesema Vee Kashera

Comments
Post a Comment