CAREEN SIMBA PACOME NI MSHKAJI TU

MREMBO Careen Simba amekana kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mchezaji Pacome  Zouzoua kama tetesi zilivyosambaa.

Careen amesema  ashangazwi na maneno ya mashabiki wala hayamuumizi kwa kuwa hata Pacome anafahamu kuwa wao ni marafiki na ni shabiki yake mkubwa.

"Pakome sio mpenzi wangu ni mchezaji wa kigeni na ni rafiki yangu mkubwa lakini pia mimi ni shabiki yake mkubwa mambo ya mapenzi ni uzushi wa mitaani" alifafanua Caren

"Maneno yanayoongelewa mitandaoni kuwa Pacome ni mpenzi wangu hayo ni maneno yao na wala hayaniumizi kichwa."

Aidha ameongeza kuwa "Bongo ukishakuwa maarufu ukaonekana na mtu fulani basi umeyaruhusu maneno kwangu ni kawaida sisi ni washikaji tu."amesema Careen Simba

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA