VIONGOZI WA DINI WAOMBA TWITTER KUFUNGIWA

 

Viongozi wa Dini nchini wamezitaka Mamlaka za serikali kuufungia mtandao wa Kijamii wa X ambao zamani ulijulikana kama Twitter Kwa kuhamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga)


Akizungumza na waandishi wa Habari leo juni 11, 2024 Jijini Dar Es Salaam Alhaj Dkt Abdul Suleiman amesema kwamba vitendo vya ushoga vimepigwa vita hata katika maandiko ya dini,hivyo vitendo hivyo havikubaliki na vinapaswa kulaaniwa.

Dkt Sule amesema kwamba kufuatia mtandao wa X (Twitter)kuruhusu kuchapisha maudhui yanayohamasisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga na usagaji Mamlaka zinazohusiana na mawasiliano zinatakiwa kuchukua hatua haraka iwezekanavyo ikiwemo kuufungia kabisa mtandao huo.

Kwa upande wake Askofu na Katibu mkuu wa Kanisa la Methodox Tanzania Allen Siso amesema katika vitabu vya dini vyote havikubaliani na ndoa za jinsia moja akitolea mfano kitabu cha Warumi 1:26 kinachosema 'hivyo Mungu aliwaacha wafuate tamaa zao za aibu,hata wanawake wakabadili matumizi ya asili Kwa matumizi yasiyo ya asili,na wanaume nao vivyo hivyo'.

Kwa upande wake Sheikh Hilal KIPOZEO amesema amesema mtandao wa X unabidi kufungiwa haraka iwezekanavyo kwani ni vyema kutengenezwa Sheria Kali ya Kudhibiti mapenzi ya jinsia moja na usagaji ili kusaidia kizazi kijacho kisiharibike.

"Mungu aliruhusu wanadamu wazaliane na wakaongezeke lakini hili tatizo hata siku moja haliwezi kuruhusu wanadamu wakazaliana na kuongezeka hivyo Mara moja mtandao wa X Ufungiwe"amesema 

Naye mwakilishi wa walimu ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Gongolamboto,Munira Njau amesema kuwa wazazi wamekuwa na tabia za kuwaachia watoto wao wachezee simu zao Hali iliyopelekea watoto kuingia kwenye mitandao hiyo na Kujifunza tabia mbaya siku Hadi siku na hatimaye kuzipeleka mashuleni.

"sisi walimu tunashinda na watoto kuanzia asubuhi mpaka jioni,na tunakutana na wanafunzi ambao tayari Wana viashiria vya tatizo hilo na tunapowahoji wanasema wamekuwa wakisema vimeanzia majumbani na wengine kupitia simu za wazazi wao,hivyo suala hili tuungane wote kusaidia watoto.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA