COSOTA YASISITIZA KAMPUNI YA WASANII WA FI LAMU
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Hakimiliki Tanzania (Cosota) Doreen Sinare amewasihi wadau wa filamu kuhakikisha wanaanzisha Kampuni za Kukusanya Mirabaha(CMOs) ili waweze kunufaika zaidi.
Tayari wasanii wa muziki wana kampuni yao ya kukusanya mirabaha iliyozinduliwa tangu mwaka jana na imeanza mchakato wa ukusanyaji ya mapato ya wasanii kwenye mitandao na vyombo vyote vinavyotumia kazi za sanaa.
Akizungumza Dar es Salaam kwenye mkutano wa wadau kukusanya maoni ya itifaki ya Beijing Sinare amesema wanategemea wasanii hao wa filamu wataanzisha kampuni yao itakayofanya kazi kwa uchungu.
"Nawadai Kampuni inayosimamia masuala ya filamu na tumebadilisha Sheria ya mwaka 2022 kuruhusu wadau wa makundi yale yanayoendana yaweze kufanya kazi zake, sisi tutakimbizana upande wa sera, kutoa elimu, kuwawekea mazingira mazuri ya sheria, kanuni na taratibu,"amesema.
Amesema:"Haya masuala ya kukusanya mirabaha inabidi myafanye nyie mtakuwa na uchungu zaidi ya sisi tunavyofanya"
Amesema wanapochelewa kuwa na kampuni hiyo, wanachelewesha maendeleo yao na Taifa hivyo wafanye kila kinachowezekana kuwa nayo.



Comments
Post a Comment