UBUNIFU WA APP YA USAFIRI MTANZAONI WAZIMA

Ubunifu Mpya wa App ya Usafiri Mtandaoni Wazima “Safari Hewa” Dar es Salaam, Tanzania – 8 Mei 2025 Katika juhudi za kukabiliana na changamoto za usalama na uaminifu kwenye sekta ya usafiri wa mtandaoni, kampuni ya Bolt Tanzania imezindua huduma mpya ya “Pick-up Code” inayolenga kuzuia safari hewa na utapeli wa kidijitali. Huduma hii huanzishwa kwa kutengeneza nambari ya siri ya usafiri (Pick-up Code) kila mara abiria anapoweka oda kupitia app. Kwa mujibu wa Meneja Mkuu wa Bolt, Bw. Dimmy Kanyankole, mfumo huu unalenga kuhakikisha safari haiwezi kuanza hadi abiria amethibitisha nambari hiyo kwa dereva aliye sahihi. “Ubunifu huu unakabiliana moja kwa moja na matatizo yanayojirudia mara kwa mara, kama vile madereva wanaoanza safari bila kumpakia abiria anayelipia kwa kadi, na pia ucheleweshaji wa safari bila sa babu za msingi,” alisema Kanyankole.
Kupitia mfumo huu, madereva halali pekee ndio watakaoidhinishwa kuendesha safari, hatua ambayo inapunguza uwezekano wa usafiri kutekelezwa na madereva bandia au wasiowaaminifu. Pia inalinda malipo ya abiria, kwani safari haiwezi kukamilishwa hadi nambari ya usafiri itakapothibitishwa. Dora Godson, mkazi wa Njiro, aliyezoea kutumia Bolt kila asubuhi kwenda kazini Burka, alisema: “Nawahi kazi sasa bila hofu. Nimewahi kudanganywa na dereva aliyebofya ‘end trip’ bila kunipakia. Hii huduma mpya inanipa ulinzi zaidi.” Takwimu kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) zinaonesha kuwa kufikia 2022, zaidi ya pikipiki 600,000 zilikuwa zimesajiliwa kwa ajili ya usafirishaji, huku idadi ya madereva wa usafiri wa mtandaoni ikiendelea kuongezeka. Hii imeongeza haja ya kuwa na mifumo madhubuti ya utambuzi na ufuatiliaji wa safari halali. Bolt inaendesha huduma hii mpya nchini Tanzania na Kenya, ikiwa ni sehemu ya dhamira yake ya kulinda usalama wa wateja na kuhakikisha malipo ya kidijitali yanazingatia viwango vya juu vya ulinzi na uwazi.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA