AZAM YAJA NA TOBOA TOBO


KAMPUNI ya Azam Media imetambulisha tamthilia ya kitanzania inazofahamika kama Toboa tobo ambayo imebeba simulizi na kuleta mapinduzi ya tasnia ya tamthilia nchini itakayoanza Februari 9 mwaka huu.


Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza amesema kuwa uzalishaji wa tamthia  hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.






Ameongeza kuwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo  kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.

Pia amesema tamthilia hiyo inachukua nafasi ya tamthilia ya Mtaa wa Kazamoyo itakayofikia tamati February 8, 2024 na Toboa tobo kuanza rasmi  February 9 2024 kuanzia Ijumaa hadi Jumapili saa moja na nusu.

Kwa upande wake mwongozaji wa tamthilia ya Toboa tobo Mayunga  amesema watanzania wakae mkao wa kula kwani tamthilia hiyo ina mengi hususani katika kutunza kuoa wake wengi na watoto kutojuana kila mtu anayo siri yake.


"Tunaanza mwezi Februari kwa kumsogeza Muhogo Mchungu na Bi Star ndani tamthilia ya Toboa tobo shughuli inaanza ya kifo cha Mzee Toboa tobo, watoto 22, na ambao walikuwa hawajulikani kufuatia marehemu Toboa Tobo kuwa na wake wanne kwa Siri huku kila mmoja akiwa hamjui mwenzake


Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA