KAMPUNI YA AZAM YAZINDUA MFUMO WA KUCHUKUA TAMTHILIA



K
AMPUNI ya Azam Media imetambulisha mfumo mpya wa upokeaji wa kazi za tamthilia ya kitanzania zinazoruka kwenye Chaneli ya Sinema Zetu kuepuka wizi wa kazi za Sanaa.


Akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam, msimamizi Mkuu wa Chaneli ya Sinema Zetu, Sophia Mgaza wakati wa uzinduzi wa mfumo huo mpya amesema kuwa uzalishaji wa tamthia  hiyo umezingatia mahitaji ya soko kwani wametumia vifaa vya uzalishaji wa kisasa na ubora wa hali ya juu,” amesema Mgaza.


Amesema awalinilikuwa unapeleka demo kwanza kwa sasa hali imekuwa nitofauti unatakiwa kuingia mtandaoni kujisajili na kujaza fomu na kuweka mikataba mbalimbali ikiwemo mwandishi wa stori vibali vya Cosota,.

Ameongeza kuwa waandaaji wapya wanaongia na kazi zao za sanaa zinazoruka kwenye chaneli hiyo  kuhakikisha wanasimamia ubora wa kazi ili wasije kutoa sababu kwa watu wa pembeni kuwanyooshea vidole na kusema kuwa ilikuwa ni nguvu ya soda tu,” amesema Mgaza.


Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA