CRDB, CCBRT WAUNGANA KUFUNGUA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WATU WENYE ULEMAVU

BENKI ya CRDB imeingia ushirikiano wa kimkakati na Hospitali ya CCBRT utakaowezesha kupanuka kwa huduma jumuishi za kifedha na kuongeza ushiriki wa watu wenye ulemavu katika shughuli za uchumi, hatua inayolenga kuondoa vikwazo vya upatikanaji wa huduma za kibenki na ajira kwa makundi yenye mahitaji maalum nchini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa kuingia makubaliano hayoMkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. AbdulMajid Nsekela, amesema makubaliano hayo yanaakisi dhamira ya benki hiyo ya kuhakikisha hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma katika mfumo wa kifedha, huku yakienda sambamba na uwekezaji katika mafunzo ya lugha ya alama kwa wafanyakazi, uboreshaji wa miundombinu ya matawi na ubunifu wa huduma zitakazokidhi mahitaji ya watu wenye ulemavu. Kwa upande wake Mkurugenzi wa CCBRT, Dk. Brenda Msangi, amesema ushirikiano huo utaijengea CRDB uwezo wa kuwa mwajiri na mtoa huduma jumuishi kupitia mafunzo ya kitaalamu, tathmini za miundombinu, maboresho ya sera na mifumo ya ajira pamoja na kuwajengea uwezo wafanyakazi kuhudumia watu wenye ulemavu kwa ufanisi na usawa.
Aidha amefafanua kuwa hatua hiyo itachochea ujumuishi wa kifedha na maendeleo ya uchumi shirikishi nchini kwa kuongeza fursa za ajira, biashara na huduma za kifedha kwa watu wenye ulemavu, huku CRDB na CCBRT zikizihimiza taasisi nyingine kuiga mfano huo ili kujenga jamii inayotoa fursa sawa za maendeleo kwa kila Mtanzania.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA