PUMA KUZINDUA PROGRAMU YA KIDIGITALI KESHO PUMA PRIS
Puma Energy Tanzania Yaendelea Kuimarisha Uchumi, Nishati Safi na Huduma za Kidijitali
Puma Energy Tanzania imeendelea kujiimarisha kama kinara wa usambazaji wa mafuta nchini kupitia uwekezaji mkubwa katika nishati, huduma za kidijitali na maendeleo ya kijamii.
Fatma Abdallah, Mkurugenzi Mtendaji Puma Energy Tanzania.Kampuni hiyo, kwa ubia na Serikali ya Tanzania, inaendesha zaidi ya vituo 100 vya huduma za mafuta nchini kote huku ikiendelea kupanua huduma za nishati safi kupitia vituo vya Gesi Asilia Iliyoshindiliwa (CNG).
Katika hatua ya kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa taifa, kampuni hiyo imeeleza kuwa inawekeza katika uvumbuzi wa kidijitali, uboreshaji wa huduma za rejareja na kuongeza upatikanaji wa nishati salama kwa wananchi na sekta mbalimbali zikiwemo usafiri, anga, kilimo na viwanda.
Mbali na kusambaza mafuta ya ndege katika viwanja vya ndege vya kimataifa na vya ndani nchini, Puma Energy Tanzania imeendelea kuonesha mchango wake kwa uchumi kwa kulipa zaidi ya shilingi trilioni 1.4 kwa Serikali kupitia kodi na ushuru katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Katika mwaka wa fedha 2023/24, kampuni hiyo ilitunukiwa tuzo mbalimbali kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania ikiwemo tuzo ya mlipa kodi mkubwa na mlipa kodi mwenye utiifu zaidi katika sekta ya mafuta na gesi.
Aidha, mwaka 2025 kampuni ilitangaza gawio la shilingi bilioni 21, hatua iliyotajwa kuongeza mapato ya Serikali kutokana na umiliki wake wa asilimia 50 kupitia Msajili wa Hazina.
Sulpis Mmasi, Meneja Mauzo ya Rejareja Puma Energy Tanzania.Katika kuimarisha huduma kwa wateja, kampuni hiyo pia imezindua programu mpya ya kidijitali ya zawadi kwa wateja ijulikanayo kama “Puma PRIS”, ikiwa ni programu ya kwanza nchini Tanzania inayowazawadia wateja wanaotumia huduma za mafuta na bidhaa za rejareja katika vituo vya kampuni hiyo.
Kupitia programu hiyo, wateja wataweza kupata pointi na zawadi wanaponunua mafuta, vilainishi na bidhaa mbalimbali, sambamba na kuhamasisha matumizi ya huduma zisizo za fedha taslimu kulingana na dira ya Tanzania ya uchumi wa kidijitali.






Comments
Post a Comment