MFUMO WA UANAGENZI (APPRENTICESHIP) WATAJWA KUFUNGUA MILANGO YA AJIRA KWA VIJANA.
Wadau wa maendeleo ya ujuzi nchini wameeleza kuwa kuimarishwa kwa mfumo wa uanagenzi (apprenticeship) unaozingatia mwongozo wa kimataifa wa mafunzo ya Uanagenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) kutasaidia kuongeza ajira kwa vijana na kuwaandaa wahitimu wenye ujuzi unaokidhi mahitaji halisi ya soko la ajira.
Hayo yamejiri katika kikao kazi kilichoandaliwa na ILO kupitia program ya ujuzi ya Dunia na msaada wa kifedha kutoka Norway cha uthibitishaji wa mpango wa utkelezaji mafunzo ya Uanagenzi (Apprenticeship Road Map) kilichofanyika mkoani Morogoro, kikiwakutanisha wadau kutoka taasisi za elimu, vyuo vya ufundi, Serikali pamoja na sekta binafsi kujadili namna ya kuboresha mfumo wa mafunzo ya kazi kwa vitendo nchini.
Akizungumza na waandihi wa habari, Albert Okal, Mshauri wa masuala ya ukuzaji ujuzi kutoka ofisi ya ILO Pretoria, amesema warsha hiyo imelenga kutathmini namna mfumo wa uanagenzi unavyoendeshwa Tanzania na jinsi unavyoendana na mwongozo wa kimataifa uliowekwa na ILO pamoja na wanachama wake.
Amesema kupitia uchambuzi wa mitaala uliofanywa na wataalamu, imebainika kuwa mfumo wa uanagenzi nchini bado haujashika kasi kama ilivyotarajiwa. “Baadhi ya taarifa tunazozipata zinaonesha kuwa uanagenzi bado haujawa sehemu kubwa ya mfumo wa mafunzo ya amali kama ilivyo kwa programu nyingine za elimu ya ufundi, hivyo tunatarajia ripoti hii itatusaidia kubaini maeneo yanayohitaji maboresho,” amesema Okal.
Kwa upande wake, Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya mafunzo ya Amali Zanzibar Dk. Bakari Ali Silima, amesema mfumo wa uanagenzi ni nyenzo muhimu ya kuhakikisha wahitimu wanapata ajira kutokana na kuandaliwa kulingana na mahitaji ya soko la kazi na viwanda.
“mafunzo ya uanagenzi yanahitajika sana katika taasisi zetu za elimu hasa vyuo vikuu, tukiweza kutoa mafunzo kama haya tunauhakikia wakutoa ajira kwa vijana watakaohitimu masomo yao na hicho ndiyo kinachotakiwa na suala la ujuzi zaidi ya mmoja ni swala ambalo linatakiwa kupewa kipaumbele”
Naye Mkurugenzi Msaidizi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia elimu ufundi na mafunzo ya ufundi stadi, Daudi Simbeye, amesema serikali imejipanga kuhakikisha mfumo huo unakuwa sehemu muhimu ya kuwasaidia vijana kupata ajira na kujiajiri.
“Waziri wa elimu sayansi na teknolojia alizindua programu ya utambuzi inayoitwa SAMIA, ambayo inasadia kutambua viajana ambao wamepata ujuzi katikaa sekta isiyo rasmi kuhakikisha kwamba wanapewa ujuzi kwenye maeneo ambayo wanahitaji kisha wanapewa vyeti ambayo vinawafanya waweze kutambulika na kuweza kujiajiri au kuajiriwa katika sekta mbalimbali”
Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu kazi, ajira na mahusiano, Dennis Assey, amesema kupitia warsha hiyo ILO imewasilisha ripoti ya tathmini (trace study) iliyochunguza hali halisi ya mfumo wa uanagenzi Tanzania kwa kuzingatia Recommendation 208.
Assey amesema serikali itaendelea kushirikiana na ILO katika kuimarisha mfumo huo kupitia programu ya taifa ya ukuzaji ujuzi, ambapo zaidi ya vijana 5,000 wanaendelea kupata mafunzo ya uanagenzi katika vyuo 46 nchini.
“Katika mwaka wa fedha 2025/26 sisi kama Ofisi ya waziri mkuu kazi ajira na mahusiano tumeweza kutekeleza programu ya taifa yakutekeleza ujuzi na eneo mopjawapo
laa programu hiyo ni mafunzo ya uanagenzi na tumewezesha jumla ya vijana zaidi ya 5000 ambao wapo vyuo mbalimbali hapa nchini wanaendelea kujifunza katika
vyuo 46 nchi na mafunzo haya sisi tunatangaza kila mwaka hivyo ni fursa kwa vijana kuendelea kufutilia na kuchangamkia fursa hii”.
MWISHO.







Comments
Post a Comment