TAMASHA LA TANZANIA YA THAMANI KUKUZA UZALENDO, SANAA NA UCHUMI WA VIJANA

Tamasha la “Tanzania ya Thamani” Kukuza Uzalendo, Sanaa na Uchumi wa Vijana Tamasha la Tanzania ya Thamani linatarajiwa kuwa jukwaa kubwa la kitaifa litakalotumia sanaa, utamaduni na ubunifu kuhamasisha uzalendo, kukuza uchumi wa vijana pamoja na kulinda misingi ya taifa kupitia kaulimbiu ya “Tunu Yetu.”
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, balozi wa tamasha hilo, Rhino Uelewa wa Sauti, amesema tamasha hilo litawakutanisha vijana wabunifu kutoka maeneo mbalimbali ya sanaa na utamaduni.
Ameeleza kuwa shughuli zitakazofanyika katika tamasha hilo ni pamoja na uimbaji, uchoraji, maonesho ya mavazi ya asili na kisasa, pamoja na sarakasi, ambapo yote yatafanyika Juni 19, 2026 katika ukumbi wa Mlimani City Conference Centre. Rhino amesema tamasha hilo pia litaambatana na utoaji wa vyeti vya heshima kwa watu na taasisi zilizofanya vizuri katika sekta mbalimbali za kijamii, sanaa na maendeleo ya vijana.
Kwa upande wake, msemaji wa tamasha hilo, Anania, amesema maandalizi yanaendelea vizuri na kwamba tamasha hilo linatarajiwa kuhudhuriwa na wasanii kutoka ndani na nje ya Tanzania, jambo litakalosaidia kuitangaza nchi kimataifa kupitia sanaa na utamaduni.

Comments

Popular posts from this blog

MATAIFA 8 KUIMBA TAMASHA LA PASAKA

PIMEA USIKU WA WANA NDOA ULIVYOFANA MSIFICHANE NA KUWEKEANA VITU

UONGOZI DHAIFU VYATAJWA KUVURUGA TAASISI ZA VIJANA